In Memoriam

Bartholemeus Leonius Langeveld Bart Langeveld

Tumkumbuke katika sala zetu
PADRE LEONIUS (Bartolomeo) Langeveld

Amezaliwa 9 Agosti 1928 katika kijiji cha
Scheveningen, Uholanzi.
Katika shule la Upper Primary padre mmoja
Mkapuchini Amideo alimwamshia Bart wazo la
kuwa mmisionari, hata mwaka 1943 Bart akaingia
Seminari ya Wakapuchini Langeweg.
30 Agosti 1949 akapokelewa kwa
Wakapuchini na kupewa jina la Leonius,
akafuata masomo ya juu, na kupata
Upadirisho 27 Juli 1956 pamoja na
wenzake tisa.
21 Mai 1959 mapadre Leonius, Zakeo, na
Novatus wakatumwa rasmi huko Tilburg kwa
kupewa rasmi Msalaba wa kazi ya
Umissionari, wakaondoka kwenda Afrika,
wakafika Dar es Salaam tarehe 5 Juni 1959,
wakaanza kujifunza Kiswahili.

Leonius alianza kazi Ruaha na Kilombero,
lakini mgongo wake ulipozidi kumsumbua
akahamia Dar es Salaam, akakaa Kibaha,
Kurasini, Msimbasi, na Mburahati.
Akamsaidia Alfeus huko Himo, akakaa
Mbagala, na 2001 akahamia Kwangulelo.
Na siku hizo za mwisho alifanya kazi katika
Emmaus: Senta ya Ukatekista, Sanya Juu.

Lakini ugonjwa ukamrudia kila mara, mpaka mwezi
Mei, tarehe 17 ameamua kwenda Uholanzi
kupimwa na mganga. Waganga wakampima na
kutafuta ni kitu gani hasa kinachomhangai
sha hata amekonda mno.
Wakafanya na picha ndani ya tumbo,
wakaona aina ya kansa ya tumbo.
Wakafanya mfululizo wa operesheni.
Mkubwa wake: usiku, akampaka mafuta ya
wagonjwa, lakini saa mbili usiku Leonius
amerudisha roho yake kwa Yesu, tarehe
5 Agosti 2005.

Familia Langeveld na Wakapuchini wa Uholanzi
na Tanzania.

of naar onze homepage